NEWS:MAKONDA ANENA WALIMU KUSAFIRI BURE

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni amesema yupo kwenye mpango wa kuwezesha walimu kusafiri bure kwenye daladala kwenda kazini kama njia ya kuwasaidia kuwahi na kuwapunguzia makali ya maisha.

Makonda ameyasema hayo wakati wa hafla ya kumuaga mke wa Rais mwl Janet Magufuli ambaye amekiri kuwa kwa sasa ana majukumu mengi hasa ya kumsaidia mheshimiwa Rais.

Sasa hapa najiuliza hawa wamiliki wa magari watakubali? Na je walimu watakuwa na unifomu au watalazimika kila wakati kuonesha vitambulisho? Na je hilo litakuwa suluhisho la kudumu? Na je watumishi wengine wao watajisikiaje ? Source Azam tv- habari ya saa 2 usiku.

0 comments: