NEC Yatoa Tamko Kuhusu Uchaguzi Wa Wabunge Arusha Mjini Na Handeni.
Na Jacquiline Mrisho-Maelezo
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza siku ya kupiga kura kwa baadhi ya
majimbo ambayo uchaguzi wake ulihairishwa kutokana na sababu mbalimbali
Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Jaji Mstaafu Damian Lubuva ametaja siku hiyo ya uchaguzi itakuwa Disemba 13, mwaka huu.
“Natoa
rai kwa Wananchi wote waliojiandikisha kama wapiga kura katika Majimbo
na Kata husika kujitokeza katika vituo walivyojiandikishia ili kuweza
kupiga kura na kuwachagua viongozi wanaowataka” amesema Lubuva.
Jaji Lubuva aliyataja majimbo hayo ambayo wananchi watapiga kura za kuchagua Wabunge kuwa ni Majimbo ya Arusha Mjini na Handeni Mjini ambapo uchaguzi wa Madiwani katika kata za Mvomero, Ipala na Nyamwilolewa nao utafanyika siku hiyo.
Aidha,
Jaji Lubuva amesisitiza kuwa, taratibu zilizotumika katika Uchaguzi
Mkuu wa Oktoba 25, 2015 mwaka ndizo zitakazotumika kwenye uchaguzi
kwenye majimbo hayo na kata hizo.
Kwa
ufupi, Jaji Lubuva alikumbushia baadhi ya taratibu hizo zikiwemo za
mpiga kura kubeba kadi yake ya kupigia kura pindi aendapo kupiga kura,
mawakala wa vyama vya siasa lazima wawepo kwenye kila kituo na pia
Maafisa Uchaguzi kufungua kituo na kufunga kwa muda uliopangwa na Tume.
Katika
Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 25 Oktoba 2015, uchaguzi wa Wabunge na
Madiwani wa Majimbo 7 pamoja na Kata 35 ulihairishwa kutokana na
sababu mbalimbali zikiwemo za vifo na vurugu.
0 comments: